انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٦

يَهْدِى بِهِ ٱللَّهُ مَنِ ٱتَّبَعَ رِضْوَٰنَهُۥ سُبُلَ ٱلسَّلَـٰمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذْنِهِۦ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ ١٦

{16} Kisha akataja ni nani anayeongolewa na Qur-ani hii, na ni nini sababu ya mja kufikia hilo. Kwa hivyo akasema, "Mwenyezi Mungu huwaongoa kwacho wenye kufuata radhi yake katika njia za salama." Yaani, mwenye kujitahidi na akawa na hima ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na dhamira yake ikawa nzuri, ataongozwa kwenye njia za salama ambazo anasalimika mwenyewe kutokana na adhabu na kumfikisha kwenye nyumba ya salama. Nayo ni kuijua haki na kuifanyia kazi kwa ujumla na kwa kina. Na anawatoa katika giza mbalimbali za ukafiri, na uzushi, na maasia, na ujinga na kughafilika, na kuwapeleka kwenye nuru ya imani, na Sunna, na utiifu, na elimu na kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na yote haya ni miongoni mwa uwongofu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ambaye alitakalo huwa, na ambalo hajalitaka haliwi "na huwaongoa kwenye njia iliyonyooka."