المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّا نَصَـٰرَىٰٓ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَهُمْ فَنَسُوا۟ حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا۟ بِهِۦ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ ٱلْعَدَاوَةَ وَٱلْبَغْضَآءَ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ ٱللَّهُ بِمَا كَانُوا۟ يَصْنَعُونَ ١٤
{14} Yaani kama tulivyochukua kwa Mayahudi ahadi na agano, vile vile tulichukua kwa wale waliosema: hakika sisi ni wale wanaomnusuru Isa bin Maryamu. Hao wakajitakasa kwa kumwamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na yale waliyoyaleta, lakini wakavunja ahadi, na wakasahau sehemu katika yale waliyokumbushwa kwayo kusahau kwa kielimu na kusahau kwa kivitendo. "Kwa hivyo tukaweka kati yao uadui na chuki mpaka Siku ya Qiyama, yaani, tuliwapa mamlaka baadhi yao juu ya wengineo, na ukawa baina yao uovu mwingi na uhasidi uliolazimu kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na kufanyiana uadui wenyewe kwa wenyewe mpaka Siku ya Qiyama. Na hili ni jambo linaloonekana kwani Wakristo hawakuliacha, na bado wako katika chuki, na uadui na utengano. "Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia yale waliyokuwa wakiyafanya" na awaadhibu juu yake.