المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَقَدْ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَـٰقَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ ٱثْنَىْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ ٱللَّهُ إِنِّى مَعَكُمْ ۖ لَئِنْ أَقَمْتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَيْتُمُ ٱلزَّكَوٰةَ وَءَامَنتُم بِرُسُلِى وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ ١٢
{12}Yeye Mtukufu anajulisha kuwa alichukua kwa Wana wa Israili agano zito na lililosisitizwa, na akataja sifa ya agano hilo na malipo yao ikiwa watalitekeleza, na dhambi zao ikiwa hawakulitimiza. Kisha akataja kwamba hawakuifanya, na akataja yale aliyowaadhibu kwayo, akasema, "Na hakika Mwenyezi Mungu alichukua agano la Wana wa Israili. Yaani, ahadi yao iliyosisitizwa, iliyo nzito, "Na tukawatumia kutokana nao wakuu kumi na wawili." Yaani, raisi na mkuu kwa yule aliye chini yake, ili awe msimamizi juu yao, mwenye kuwahimiza kufanya yale waliyoamrishwa, akiwataka na kuwalingania. "Na Mwenyezi Mungu akasema," akiwaambia wakuu hao ambao walibeba yale waliyobeba miongoni mwa mizigo ya majukumu. "Kwa yakini Mimi niko pamoja nanyi," yaani kwa msaada na nusura, kwani, msaada ni kulingana na mzigo wa majukumu. Kisha akataja yale aliyowachukulia agano, akasema, "Mkisimamisha Swala" kwa nje na kwa ndani kwa kufanya yanayolazimu na yanayofaa ndani yake na kudumu juu ya hayo, "na mkatoa Zaka" kwa wanaoistahiki. "Na mkawaamini Mitume wangu" wote ambao mbora wao zaidi na mkamilifu wao zaidi ni Muhammad - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani.- "Na mkawasaidia," yaani mkawatukuza na kuwatekelezea yale wanayopaswa kufanyiwa kama vile heshima na utiifu. "Na mkamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri," ambao ni sadaka na wema unaotokana na ukweli na kumkusudia Mwenyezi Mungu tu, na mapato mazuri. Basi Mkifanya hivyo, "hapana shaka nitawafutia mabaya yenu na nitawaingiza katika mabustani yapitayo mito chini yake." Basi inawaunganishia kupata kinachopendwa kwa kuwaingiza Peponi na neema iliyomo ndani yake, na kuwaepusha yanayochukiza kwa kuwafutia mabaya na kuzuia yale yanayotokana nayo miongoni mwa adhabu mbalimbali. "Kwa hivyo mwenye kukufuru miongoni mwenu baada ya hayo," yaani, ahadi na agano vilivyosisitizwa kwa viapo na kukubali majukumu kulikofungamana na kutia moyo kwa kutaja malipo yake; "basi bila ya shaka atakuwa amepotea njia iliyo sawa." Yaani, kwa makusudi na kwa kujua, kwa hivyo anastahiki yale wanayostahiki wapotevu miongoni mwa kunyimwa thawabu na kupata adhabu.