انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠٥

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا ٱهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ١٠٥

{105} Yeye Mtukufu anasema; "Enyi mlioamini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu;" yaani, jitahidini katika kuzifanya zitengenee, na kuzikamilisha, na kuzilazimisha kufuata njia iliyonyooka. Kwani, Ikiwa nyinyi mtatengenea, hatawadhuru mwenye kupotea njia iliyonyooka na wala hakuongoka kwenye Dini iliyo madhibuti, bali anajidhuru nafsi yake. Na hili haliashirii kuwa kuamrisha mema na kukataza maovu hakumdhuru mja kwa kuyaacha au kuyapuuza. Kwani uwongofu wake haukamiliki isipokuwa kwa kuyafanya yale ambayo ni wajibu juu yake miongoni mwa kuamrisha mema na kukataza maovu. Ndiyo; ikiwa hawezi kuyakemea maovu kwa mkono wake na ulimi, na akayachukia kwa moyo wake, basi hakumdhuru kupotea kwa wengineo. Na kauli yake: "Ni kwa Mwenyezi Mungu ndiyo marejeo yenu nyote." Yaani, maishio yenu siku ya Kiyama na kukusanyika kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; "kisha atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda," miongoni mwa mema na mabaya.