المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَسْـَٔلُوا۟ عَنْ أَشْيَآءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْـَٔلُوا۟ عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلْقُرْءَانُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا ٱللَّهُ عَنْهَا ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ١٠١
{101} Anawakataza waja wake Waumini kuuliza kuhusu mambo ambayo wakibainishiwa, yatawawiya mabaya, na kuwahuzunisha. Na hayo ni kama vile maswali ya baadhi ya Waislamu walipomuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - kuhusu baba zao, na kuhusu hali yao ya Peponi au Motoni. Kwa hivyo, hili huenda lau lingebainishwa kwa muulizaji, basi hangekuwa na heri yoyote ndani yake. Na kama vile kuuliza kwao mambo ambayo hayawezi kutokea, na kama vile swali ambalo linasababisha kufanyiwa ugumu katika Sheria ambalo huenda likawaletea umma ugumu; kama vile kuuliza juu ya mambo yasiyomhusu. Basi maswali haya na mfano wake ndiyo yamekatazwa. Na ama swali ambalo halisababishi chochote katika hayo, basi hilo limeamrishwa kufanywa hivyo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu; "Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui." "Na mkiuliza juu yake wakati inateremshwa Qur-ani, mtadhihirishiwa hayo;" yaani, ikiwa swali lenu litaafikiana na pahali pake, na mkauliza juu yake wakati inapoteremshwa Qur-aani kwenu. Kama mkiuliza kuhusu Aya inayowatatiza au hukumu ambayo sababu yake imefichikana kwenu, katika wakati ambao wahyi unaweza kuteremka kutoka mbinguni "mtadhihirishiwa hayo." Yaani, itabainishwa kwenu na kudhihirishwa, na vinginevyo; nyamazeni kimya juu ya kile ambacho Mwenyezi Mungu alikinyamazia kimya. "Mwenyezi Mungu ameyasamehe hayo;" yaani, alinyamaza na kuwaachia waja wake hilo. Basi kila jambo ambalo mwenyezi Mungu alilinyamazia, basi hilo ni katika yale aliyoyaruhusu na kuyasamehe. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole;" yaani, hajaacha kusifika kwa kufuta dhambi, na kwa kujulikana kwa Upole na ihsani. Basi kuendeeni kufutiwa dhambi kwake na ihsani yake, na tafuteni katika rehema yake na radhi zake kutoka kwake.