الجاثية
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَهُ ٱلْكِبْرِيَآءُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ ٣٧
{37} "Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi." Yaani, ni wake utukufu, ukuu na heshima kubwa. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu anasifika kwa sifa njema za ukamilifu, anapendwa na anatukuzwa. Na pia Yeye ni mwenye ukubwa, ukuu na heshima kubwa mno. Kwani, ibada imejengwa juu ya nguzo mbili: kumpenda Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea. Na mawili hayo yanatokana na kujua sifa njema za Mwenyezi Mungu, utukufu wake na ukubwa wake. "Naye ni Mwenye nguvu," aliyeshinda kila kitu. "Mwenye hekima," anayeweka vitu mahali pake pa sawasawa. Kwa hivyo, hawezi kuweka sheria alizoweka isipokuwa kwa hekima na masilahi, na wala haumbi anachokiumba isipokuwa kwa masilahi na manufaa.
Imekamilika tafsiri ya surat Al-Jathiya, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na neema na fadhila.