انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الجاثية
السورة ٤٥

الجاثية

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٧

وَءَاتَيْنَـٰهُم بَيِّنَـٰتٍ مِّنَ ٱلْأَمْرِ ۖ فَمَا ٱخْتَلَفُوٓا۟ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِى بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ١٧

{17} "Na tukawapa" Wana wa Israili "maelezo wazi" yanayobainisha haki kutokana na batili "ya amri" inayohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu aliwafikishia. Na maelezo hayo ni miujiza waliyoiona kupitia mkono wa Musa, amani iwe juu yake. Neema hizi alizowapa Mwenyezi Mungu Wana wa Israili zilihitaji wazitekeleze kwa ukamilifu kabisa, na kwamba waungane juu ya haki ambayo Mwenyezi Mungu aliwabainishia. Lakini jambo hilo likawa kinyume, wakayafanyia kinyume na inavyolazimu, na wakahitilafiana katika yale waliyoamrishwa kuungana ndani yake, na ndiyo maana akasema: "Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia na elimu;" yaani, inayofanya wasitofautiane. Na kilichowafanya kutofautiana ni ukandamizaji na dhuluma ya wenyewe kwa wenyewe. "Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitalifiana" ili apambanue aliye kwenye haki na aliye katika batili, na apambanue aliyehitilafiana kwa sababu ya matamanio au kitu chenginecho.