الجاثية
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
هَـٰذَا هُدًى ۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ ١١
{11} Alipofafanua ishara zake za ki Qur-ani na za kuonekana kwa macho, na kwamba watu katika hizo wamegawanyika makundi mawili, akajulisha kwamba Qur-ani hii inayojumuisha mambo haya makubwa ni uwongofu. Akasema: "Huu ni uwongofu." Haya ni maelezo ya jumla ya Qur-ani yote. Kwa maana inaongoza kwenye kumjua Mwenyezi Mungu kwa sifa zake takatifu na matendo yake yenye kusifiwa, na inaongoza kwenye kuwajua Mitume wake, vipenzi wao na maadui zao na sifa zao, na inaongoza kwenye matendo mema, na inalingania kwa hayo na kubainisha matendo mabaya na kuyakataza, na inaongoza katika kubainisha malipo ya matendo, na inabainisha malipo ya duniani na akhera. Kwa hivyo, wale walioongoka waliongoka kwayo, nao basi wakafanikiwa na kuwa na furaha. "Na wale wale waliozikataa Ishara za Mola wao Mlezi" zilizo wazi wazi na za uhakika kabisa, ambazo hakuna mwenye kuzikataa isipokuwa mwenye dhuluma kubwa mno na ukazidi upotofu wake, "watapata adhabu inayotokana na ghadhabu, iliyo chungu."