الزخرف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَمْ أَبْرَمُوٓا۟ أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ ٧٩
{79} Mwenyezi Mungu Mtukufu "Au" hao walioikadhibisha haki na kuipinga "waliweza kupitisha amri yao?" Yaani, walipanga vitimbi na wakapanga njama dhidi ya haki na yule aliyeileta haki hiyo ili waiangushe kwa yale waliyoficha ya batili iliyopambwa. "Bali ni Sisi ndio tunaopitisha." Yaani, tunalifanya jambo letu kuwa sawasawa na kulipanga mpango unaopita mpango wao, na kuupindua na kuubatilisha. Na hayo ni zile sababu na ushahidi ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliviweka kwa ajili ya kuisimamisha haki na kubatilisha batili. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka."