الزخرف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَنَادَوْا۟ يَـٰمَـٰلِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّـٰكِثُونَ ٧٧
{77} "Nao watapiga kelele waseme" na hali wamo Motoni wakitaraji kupumzishwa. "'Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi!'" Yaani, basi na tufishe ili tupumzike. Kwani sisi tumo katika huzuni kubwa sana na adhabu kali sana, ambayo hatuwezi kusubiri juu yake wala kustahimili. Basi "aseme" Malik, mlinzi wa Moto walipomwomba awaombee kwa Mwenyezi Mungu awaangamize: "'Hakika nyinyi mtakaa humo humo!'" Na kamwe hamtatoka. Kwa hivyo hawakuyafikia yale waliyoyakusudia. Bali aliwajibu kwa yaliyo kinyume na makusudio yao, na akawaongezea huzuni kubwa juu ya huzuni yao.