انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزخرف
السورة ٤٣

الزخرف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٣

وَلَمَّا جَآءَ عِيسَىٰ بِٱلْبَيِّنَـٰتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِٱلْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ ٱلَّذِى تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ٦٣

{63} "Na alipokuja Isa na hoja zilizowazi" zinazoashiria ukweli wa unabii wake na usahihi wa yale aliyowaletea kama vile kufufua wafu na kuponya vipofu na wakoma na ishara nyinginezo, "alisema" akiwaambia Wana wa Israili: "'Nimekukujieni na hekima'", yaani unabii na elimu ya yafaayo kwa namna inavyofaa, "na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyokhitalifiana." Yaani, nitakubainishieni usahihi wake na jawabu lake, ili kwa hayo mkanganyiko uondoke. Basi yeye, amani iwe juu yake, akaja katika hali ya kukamilisha na kuitimiza sheria ya Musa, amani iwe juu yake, na hukumu za Taurati, na akaleta baadhi ya wepesishaji uliohitaji kumfuata na kukubali yale aliyokuja nayo. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii mimi." Yaani, mwabuduni Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika, tekelezeni amri zake, jiepusheni na makatazo yake, niaminini mimi, mnisadiki na mnitiini.