الزخرف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالُوٓا۟ ءَأَـٰلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًۢا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ ٥٨
{58} "Wakasema: 'Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu?'" Yaani, Isa (Yesu); ambapo ilikuwa imekatazwa kuviabudu vyote, na ikatolewa ahadi ya adhabu kwa anayeviabudu, na pia ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu." Msingi wa hoja yao ya dhuluma ni kuwa walisema: 'Imethibiti kwetu na kwenu ewe Muhammad, ya kwamba Isa ni miongoni mwa waja wa karibu muno na Mwenyezi Mungu, ambaye atakuwa na mwisho mwema. Basi kwa nini ulisawazishe baina yake na masanamu katika kukataza kuviabudu vyote? Kama hoja yako haikuwa batili, basi haingepingana hivi. Na kwa nini ulisema: "'Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu?" Maneno haya, kulingana na madai yao, yanajumuisha masanamu na Isa. "Basi je, huku si chochote ila ni kupingana? Na kupingana kwa hoja ni ushahidi wa ubatili wake!" Hii ndiyo hoja kubwa zaidi wanayothibitisha kwayo fikira hii potofu na ambayo ndiyo batili zaidi ya hoja zote. Basi waliifurahia hoja hii na wakawa kupiga kelele kwa sababu yake na kupokezana habari njema. Lakini hii - sifa njema ni za Mwenyezi Mungu - ni katika fikira potofu, dhaifu na batili zaidi. Kwa maana, kusawazisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kati ya kukataza kumuabudu Masihi na kukataza kuabudu sanamu ni kwa sababu ibada ni haki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hakuna anayeistahiki katika viumbe, si Malaika walio karibu naye, wala Manabii waliotumwa, wala yeyote asiyekuwa wao katika viumbe. Je, kuna suala lolote la utata kwenye kusawazisha kati ya kumwabudu Isa na visivyokuwa yeye?