انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٧

فَٱصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ ۚ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ ٧٧

{77} Yaani, "basi subiri" ewe Mtume juu ya kulingania watu wako na maudhi yanayokusibu kutoka kwao, na usubiri kwa msaada wa imani yako. "Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli." Atainusuru dini yake na kuliinua juu neno lake, na atawapa ushindi Mitume wake katika dunia na Akhera.Tafuta msaada juu ya hilo kwa kujua kwamba maadui zako wataadhibiwa duniani na Akhera. Na ndiyo maana akasema: "Na ama tukikuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi" katika dunia, "au tukikufisha" kabla ya kuwaadhibu, "basi kwetu tu ndiko watarudishwa." Kisha tutawalipa kwa matendo yao. Basi kamwe usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayoyafanya madhalimu.