انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٥

ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمْ تَفْرَحُونَ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَمْرَحُونَ ٧٥

{75} Na wataambiwa watu wa Motoni: "Hiyo" adhabu mliyopewa ya anuwai "ni kwa sababu mlikuwa mkijitapa katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijishaua." Yaani, mlikuwa mkifurahia batili yenu na elimu mliyopingana nayo, elimu ya Mitume, na mnajishaua juu ya waja wa Mwenyezi Mungu kwa dhuluma, kuvuka mipaka na uasi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu mwishoni mwa Sura hii: "Basi Mitume wao walipowajia kwa ushahidi ulio wazi, walijitapa kwa elimu waliyokuwa nayo." Na kama vile watu wa Qaruni walivyomwambia: "Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba." Hii ndiyo furaha inayokatazwa ambayo inasababisha mtu kuadhibiwa, tofauti na furaha inayosifiwa ambayo Mwenyezi Mungu alisema kuhusiana nayo: "Sema: 'Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo." Ambayo ni kufurahia elimu yenye manufaa na matendo mema.