غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَخَلْقُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ٥٧
{57} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha yaliyothibiti katika akili kwamba "kuumba mbingu na ardhi" pamoja na ukubwa wake na upana wake "ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu." Kwa maana, kwa kulinganisha na uumbaji wa mbingu na ardhi, ni vitu vidogo zaidi. Kwa hivyo, Yule aliyeumba miili mikubwa na akaifanya kuwa sawasawa ana uwezo zaidi na anafailia zaidi kuwarudisha watu baada ya kufa kwao. Huu ni katika ushahidi wa kiakili unaoonyesha ufufuo kwa njia ya uhakika mara tu mwenye akili anapoutazama na akautumia kama ushahidi usio na shaka yoyote wala fikira potofu kwamba yatatokea yale ambayo Mitume walijulisha kuhusu ufufuo. Siyo kila mtu anaiweka akili yake katika hilo na akalitafakari. Ndiyo maana akasema: "Lakini watu wengi hawajui," ndiyo maana hawayazingatii hayo wala hawayaweki maanani.