انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَٱلْأَحْزَابُ مِنۢ بَعْدِهِمْ ۖ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍۭ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ ۖ وَجَـٰدَلُوا۟ بِٱلْبَـٰطِلِ لِيُدْحِضُوا۟ بِهِ ٱلْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ ٥

{5} Kisha akawatishia wale wanaojadili Aya za Mwenyezi Mungu ili wazibatilishe, kama walivyofanya wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa kaumu mbalimbali kama vile "kaumu ya Nuhu" na 'Adi "na makundi mengine baada yao" ambayo yalijipanga makundi na wakakusanyika dhidi ya haki ili waipindue na wakakusanyika juu ya batili ili waiunge mkono. "Na" kwamba hali yao hiyo na makundi yao hayo yaliwafikisha kiwango kwamba "kila taifa lilikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate" na wamuue. Hili ndilo jambo la kubwa zaidi wanaloweza kuwafanyia Mitume, ambao ndio viongozi wa watu wema, ambao wako katika haki safi, isiyo na shaka yoyote wala utata. Basi je, kuna chochote baada ya uasi huu, upotofu huu, kuwa mashakani huku isipokuwa adhabu kubwa ambayo hawataepukana nayo? Ndiyo sababu akasema katika adhabu yao ya kidunia na ya kiakhera: "Kwa hivyo niliwakamata" kwa sababu ya kukadhibisha kwao na kujiweka kwao makundi. "Basi ilikuwaje adhabu yangu!" Ilikuwa adhabu kali na mbaya zaidi. Haikuwa isipokuwa ukelele mmoja tu au kushukiwa na tufani ya changarawe au kuiamuru ardhi ikawadidimiza kuzamishwa baharini, basi wakawa wamezimika.