غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَسَتَذْكُرُونَ مَآ أَقُولُ لَكُمْ ۚ وَأُفَوِّضُ أَمْرِىٓ إِلَى ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَصِيرٌۢ بِٱلْعِبَادِ ٤٤
{44} Alipowanasihi, akawatahadharisha na akawaonya, lakini hawakumtii wala hawakukubaliana naye, akawaambia: "Basi mtayakumbuka ninayokuambieni" katika nasaha hii na mtaona madhara ya kutoikubali itakapokufikieni adhabu, na mtakaponyimwa ujira mkubwa. "Nami ninamkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu." Yaani, ninamkimbilia na kushikamana naye, na kumuachia mambo yangu yote, na kumtegemea Yeye katika kunifikishia masilahi yangu na kuniepushia madhara yanayonipata kutoka kwenu au kutoka kwa wasiokuwa nyinyi. "Hakika Mwenyezi Mungu anawaona vyema waja wake." Anazijua hali zao na wanayostahiki. Anaijua hali yangu na udhaifu wangu, basi ananilinda kutokana nanyi na ananitosheleza na shari yenu. Na anazijua hali zenu, basi hamuwezi kutenda chochote ila kulingana na utashi wake na mapenzi yake. Kwa hivyo, akikupeni mamlaka juu yangu, basi ni kwa sababu ya hekima yake Mtukufu, na kwa utashi wake na mapenzi yake.