غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَقَدْ جَآءَكُمْ يُوسُفُ مِن قَبْلُ بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَمَا زِلْتُمْ فِى شَكٍّ مِّمَّا جَآءَكُم بِهِۦ ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَن يَبْعَثَ ٱللَّهُ مِنۢ بَعْدِهِۦ رَسُولًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُّرْتَابٌ ٣٤
{34} "Na alikwishawajieni Yusuf" mwana wa Yaaqub, amani iwe juu yao wote wawili, "zamani" kabla ya kuja kwa Musa na ushahidi wa wazi unaoonyesha ukweli wake, na akakuamrisheni kumwabudu Mola wenu Mlezi peke yake, bila mshirika yeyote. "Lakini nyinyi mliendelea katika shaka kwa yale aliyokuleteeni" katika uhai wake, "mpaka alipokufa" shaka yenu hiyo na ushirikina wenu vikazidi, "mkasema: Mwenyezi Mungu hataleta kabisa Mtume baada yake." Yaani, hii ilikuwa ndiyo dhana yenu batili ambayo haimfailii Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hawezi kuwaacha bure viumbe wake, bila ya kuwaamrisha na kuwakataza, bali huwatumia Mitume wake. Na kudhani kuwa Mwenyezi Mungu hatamtuma Mtume ni upotofu, na ndiyo maana akasema: "Kama hivyo Mwenyezi Mungu humpoteza yule anayepindukia mipaka katika maasi, anayejitia shaka." Hivi ndivyo walivyomuelezea Musa kwa uhakika, ambayo ni maelezo ya kidhuluma na ukaidi. Kwani wao ndio waliopindukia mipaka haki na wakauendea upotofu. Nao ni waongo kwa kuwa walimnasibisha Mwenyezi Mungu na hayo na wakamkadhibisha Mtume wake. Na anayesifika kwa kupitiliza mipaka na uwongo hawezi kuachana na hayo, na wala Mwenyezi Mungu hamwongoi wala hamwezeshi kufikia heri kwa sababu aliikataa haki baada ya kumfikia na akaijua. Kwa hivyo, malipo yake ni kwamba Mwenyezi Mungu anamuadhibu kwa kumnyima uwongofu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Walipopotoka, Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao." Na kauli yake: "Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyokuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga." Na kuali yake: "Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu."