غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَـٰقَوْمِ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ يَوْمَ ٱلتَّنَادِ ٣٢
{32} Alipowahofisha juu ya adhabu za duniani, akawahofisha pia juu ya adhabu ya Akhera, akasema: "Na enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia Siku ya mayowe" huko Akhera ambapo wakazi wa Bustani ya mbinguni watakapowaita wakazi wa Motoni: "Sisi tumekuta yale aliyotuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli." Mpaka mwisho wa Aya "Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi: Tumiminieni maji au chochote alichokuruzukuni Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharamisha hivyo kwa makafiri." Na wakati wakazi wa Motoni watakapomwita Malik, mlinzi wa Jahannam: "Na atufishe Mola wako Mlezi!" naye atasema: "Hakika nyinyi mtakaa humo humo!" Na watakapomwita Mola wao Mlezi: "Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tukiyarejelea tena, basi kweli sisi ni wenye kudhulumu." Basi atawajibu: "Tokomeeni humo, wala msinisemeshe." Na watakapoambiwa washirikina: "Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu! Basi watawaita, lakini hawatawaitikia."