غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالَ مُوسَىٰٓ إِنِّى عُذْتُ بِرَبِّى وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لَّا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ ٱلْحِسَابِ ٢٧
{27} "Na Musa akasema" wakati Firauni alipoyasema maneno hayo mabaya ambayo dhuluma yake ndiyo ilimfanya kuyasema, basi Musa akatumia nguvu zake na uwezo wake na akamuomba msaada Mola wake Mlezi: "Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi," ambaye kwa umola wake huo anaendesha mambo yote, "anilinde na kila mwenye jeuri asiyeiamini Siku ya Hesabu." Yaani, ambaye kiburi chake na kutoiamini kwake Siku ya Hesabu vinamfanya kutenda maovu na uharibifu. Haya anaingia ndani yake Firauni na wengineo, kama ilivyotajwa hapo nyuma katika kanuni ya hapo awali. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa upole wake akamzuia mbali na kila mwenye jeuri asiyeiamini Siku ya Hesabu, na akamuwekea visababu ambavyo kwavyo alizuilika kutokana na ubaya wa Firauni na wakuu wake na dhulma yao.