انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٠

وَٱللَّهُ يَقْضِى بِٱلْحَقِّ ۖ وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَقْضُونَ بِشَىْءٍ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْبَصِيرُ ٢٠

{20} "Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki." Kwa sababu kauli yake ni haki, na hukumu yake ya kisheria ni haki, na hukumu yake ya kimalipo ni haki. Naye amedhibiti kila kitu kwa elimu, na kuandika na kukihifadhi. Naye ametakasika mbali na dhuluma, upungufu na kasoro zinginezo zote. Naye ndiye anayepitisha mipangilio yake ya mambo yote, ambaye anapotaka jambo, linakuwa. Na kile ambacho hakitaki, hakiwi. Naye ndiye anayehukumu baina ya waja wake waumini na makafiri katika dunia hii na kuwatenganisha kwa kuwapa ushindi marafiki zake na vipenzi wake. "Lakini hao wanaowaomba badala yake hawahukumu chochote" kwa sababu ya kutoweza kwao, na kwamba hawana utashi juu ya heri na uwezo wa kuifanya. "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia" sauti zote kwa lugha mbalimbali na mahitaji mbalimbali. "Mwenye kuona" yaliyokuwepo, yatakayokuwepo, na yanayoonekana na yasiyoonekana, na yale ambayo waja wanayajua na wasiyoyajua. Alisema katika aya ya kwanza katika aya hizi mbili: "Na waonye siku inayokurubia," kisha akaielezea kwa sifa hizi zinazohitaji kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo kuu; kwa sababu inajumuisha mambo ya kutia moyo na vitisho.