انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ ٱلْـَٔازِفَةِ إِذِ ٱلْقُلُوبُ لَدَى ٱلْحَنَاجِرِ كَـٰظِمِينَ ۚ مَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ ١٨

{18} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad, rehema na amani zimshukie: "Na waonye siku inayokurubia," na ambayo umefika wakati wa hali zake ngumu, wasiwasi wake mkubwa na mitetemeko yake. "Wakati nyoyo zitakapofika kooni" na macho yao yakawa yamekodoka kwa sababu ya hofu kubwa na dhiki, "nao wamejaa huzuni" kwa sababu ya yale yaliyo ndani ya nyoyo zao ya hofu kubwa na mambo makubwa yanayowasumbua. Hawatasema ila yule ambaye Mwingi wa rehema atamruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. "Madhaalimu hawatakuwa na rafiki" wala jamaa wa karibu, "wala mwombezi wa kuitikiwa." Kwa sababu waombezi hawamuombei yule aliyejidhulumu nafsi yake kwa ushirikina, na hata kama ingechukuliwa kwamba wataweza kufanya uombezi,Mwenyezi Mungu haridhii uombezi wao huo, kwa hivyo hataukubali.