غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ ٱللَّهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى ٱلْإِيمَـٰنِ فَتَكْفُرُونَ ١٠
{10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu fedheha na hizaya itakayowapata makafiri na maombi yao ya kurejea na kutoka Motoni, na kutowezekana kwa hayo: "Hakika wale waliokufuru." Hili linajumuisha kila aina ya ukafiri, kama vile kumkufuru Mwenyezi Mungu, au vitabu vyake, au Mitume wake, au Siku ya Mwisho. Hilo litatokea watakapokuwa wanaingia Motoni na wakakiri kuwa wanaustahiki kweli kwa sababu ya dhambi na makosa waliyoyafanya. Hapo, watajichukia nafsi zao na kuzikasirikia sana, kisha wanaitwa na kuambiwa: "Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu." Mlipokuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mnakufuru. Wakati Mitume na wafuasi waliwaita ili muamini, na wakawasimamishia hoja zilizo wazi ambazo kwazo haki ilibainika, lakini mkakufuru na mkakata tamaa ya kuamini jambo ambalo Mwenyezi Mungu alikuumbieni kwa ajili yake, na mkatoka katika rehema yake pana, kwa hivyo akakuchukieni. Hayo ni kitu "kikubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu." Basi hali yenu hii iliendelea kuwa hivi kwa hivyo akawachukia na kuwakasirikia, mpaka leo mmepatwa na ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wakati Waumini walipata radhi na malipo ya Mwenyezi Mungu.