النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّـٰلِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُو۟لَـٰٓئِكَ رَفِيقًا ٦٩
{69} Yani kila mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kulingana na hali yake, na kwa kiasi cha wajibu ulio juu yake, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa. "Basi hao wako pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu" kwa neema kubwa inayolazimu ukamilifu, na kufaulu, na furaha. "Miongoni mwa Manabii" ambao Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha kwa wahyi wake na akawateua kwa kuwaboresha kwa kuwatuma kwa viumbe na kulingania kwao kwa Mwenyezi Mungu. "Na Wakweli". Nao ndio wale ambao kulikamilika kusadiki kwao yale waliyoyaleta Mitume. Kwa hivyo wakaijua haki na wakaiamini kwa yakini yao na kwa kuitenda kwa kauli, na vitendo, na hali na kulingania kwa Mwenyezi Mungu. "Na mashahidi" ambao walipigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu ili kuliinua Neno la Mwenyezi Mungu, na wakauawa. "Na walio wema" ambao ilitengenea dhahiri yao na ndani yao, basi matendo yao yakatengenea. Kwa hivyo, kila mwenye kumtii Mwenyezi Mungu, atakuwa pamoja na hawa, na katika wenza wao. "Na hao ndio wenza wazuri zaidi" kwa kujumuika nao katika Mabustani yenye neema, na kupata utulivu kwa kuwa karibu nao katika ujirani wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.