النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَمْ يَحْسُدُونَ ٱلنَّاسَ عَلَىٰ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۖ فَقَدْ ءَاتَيْنَآ ءَالَ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَءَاتَيْنَـٰهُم مُّلْكًا عَظِيمًا ٥٤
{54} “Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake?” Yani je, kilichowafanya kusema waliyoyasema ni kuwa wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu, basi wanamboresha wamtakaye? Au kilichowafanya kutenda hivyo ni husuda kwa Mtume na kwa Waumini kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake? Na hilo si jambo geni wala si la ajabu kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu. “Basi hakika tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hekima, na tukawapa ufalme mkubwa.” Na hayo aliyompa Ibrahimu na kizazi chake miongoni mwa unabii, na Kitabu, na ufalme, ndiyo aliyowapa wale aliowapa miongoni mwa Manabii wake, kama vile Daudi na Sulemani. Kwa hivyo, neema yake haijaacha kuendelea juu ya waja wake Waumini. Basi vipi wanakanusha neema yake kwa utume, na nusura, na utawala kwa Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - mbora zaidi wa viumbe vyote, na mtukufu wao zaidi, mkubwa wao zaidi katika kumjua Mwenyezi Mungu, na amnyenyekeaye wao zaidi?