النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱنظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثْمًا مُّبِينًا ٥٠
{50} Yeye Mtukufu alisema, "Tazama namna wanavyomzulia uwongo Mwenyezi Mungu" Yani kwa kujitakasa nafsi zao. Kwa sababu, hili ni katika uzushi mkubwa zaidi dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, yaliyomo ndani ya kujitakasa kwao huko ni kujulisha ya kwamba Mwenyezi Mungu aliifanya hali waliyo nayo kuwa ndiyo haki, na hali waliyo nayo Waumini kuwa ndiyo batili. Na huu ni uwongo mkubwa zaidi, na kugeuza uhakika kwa kuifanya haki kuwa batili, na batili kuwa haki. Na kwa sababu hii ndiyo akasema, "na hilo linatosha kuwa dhambi iliyo wazi." Yani lililo dhahiri, wazi, lenye kusababisha mateso yenye kuingia, na adhabu chungu.