النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ نَصِيبًا مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ يَشْتَرُونَ ٱلضَّلَـٰلَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا۟ ٱلسَّبِيلَ ٤٤
{44} Hii ni kashfa kwa wale “waliopewa fungu katika Kitabu.” Na ndani yake kuna tahadharisho kwa waja wake dhidi ya kudanganywa nao, na kuingia katika mitego yao. Kwa hivyo, akajulisha kwamba wao wenyewe “wananunua upotovu.” Yani wanaupenda upendo mkubwa, na wanaupendelea upendeleo wa mwenye kutoa mali nyingi katika kutafuta kile anachokipenda. Basi wanaupendelea upotovu kuliko uwongofu, na ukafiri kuliko imani, na taabu kuliko furaha, na pamoja na haya “wanataka kwamba mpotee Njia,” Hivyo basi, wao wanafanya hima kubwa sana kuwapoteza, wakifanya juhudi zao katika hilo. Lakini kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wa waja wake Waumini na mwenye kuwanusuru, akawabainishia yale wanayojumuisha miongoni mwa upotovu na upotoshaji.