انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٢

يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَعَصَوُا۟ ٱلرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ ٱلْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ ٱللَّهَ حَدِيثًا ٤٢

{42} Ndiyo maana akasema, “Siku hiyo watapenda wale waliokufuru na wakamuasi Mtume.” Yani waliokusanya kati ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kumuasi Mtume. “Lau kuwa ardhi isawazishwe kwao,” yani iwameze ili wawe vumbi na wasiwe kitu. Kama vile alivyosema Yeye Mtukufu, “na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa udongo!” “Wala hawataweza kumficha Mwenyezi Mungu neno lolote.” Yani watamkiria yale waliyoyatenda, na vitashuhudia dhidi yao ndimi zao, na mikono yao, na miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyafanya. Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawalipa kikamilifu malipo yao ya haki. Na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye wa haki, Mwenye kudhihirisha. na wanajua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi. Ama yale yaliyokuja kwamba makafiri wataficha ukafiri wao na kukanusha kwao, hayo kwa hakika yatatokea katika baadhi ya sehemu za Qiyama watakapodhani kuwa kukanusha kwao, kutawanufaisha kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na watakapojua uhakika wa mambo, na viungo vyao vikashuhudia dhidi yao, hapo jambo hilo litadhihirika wazi, na hakutakuwa na mahali pa kufichika, wala hakutanufaisha wala kufaidi.