انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٥

وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَٱبْعَثُوا۟ حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِۦ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصْلَـٰحًا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيْنَهُمَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ٣٥

{35} Yani ikiwa mnahofia kuwepo mfarakano baina ya wanandoa wawili, na kujiweka mbali, na kujiepusha mpaka akawa kila mmoja wao katika upande tofauti “basi mtumeni mpatanishi kutoka kwa jamaa za mume, na mpatanishi kutoka kwa jamaa za mke.” Yani wanaume wawili wanaojukumishwa kisheria, Waislamu, waadilifu, wenye akili timamu, wanaojua yaliyo baina ya wanandoa hao, na wanajua kuunganisha na kutenganisha. Na haya yanafahamika kutokana na neno ‘mpatanishi.’ Kwa sababu, hafai kuwa mpatanishi isipokuwa yule anayesifika kwa sifa hizo. Kwa hivyo, wataangalia yale ambayo kila mmoja wao anakichukia kwa mwenzake, kisha wanamlazimisha kila mmoja wao kutekeleza wajibu wake. Ikiwa mmoja wao hawezi kufanya hivyo, wanamshawishi mwenzi wake kuridhika na kile chepesi kilichowezekana katika riziki na maadili. Na chochote ambacho wataweza kuunganisha na kurekebisha, basi wasikiache. Na iwapo hali itafikia kwamba haiwezekani kuwaunganisha na kuwarekebisha isipokuwa kwa njia ya uadui, na kutengana, na kumuasi Mwenyezi Mungu, na wakaona kwamba kutenganisha baina yao ndiyo bora zaidi, basi watatenganisha baina yao. Wala haihitajiki ridhaa ya mume, kama inavyoashiriwa na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaita ‘wapatanishi wawili,’ naye mpatanishi anaweza toa hukumu hata kama aliyehukumiwa hataridhia. Na ndiyo maana akasema, “Ikiwa wanataka kutengeneza mambo, Mwenyezi Mungu atawawezesha kati yao.” Yani, kwa kuwapa maono mazuri na maneno yanayovutia nyoyo na yanaunganisha baina ya makundi mawili hayo. “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari zote.” Yani anajua ya dhahiri yote na ya ndani yote, na anayajua yaliyofichikana ya mambo yote na siri zake. Ni katika kujua kwake na kuwa kwake na habari zote ni kwamba alikuwekea hukumu hizi tukufu na sheria hizi nzuri.