انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣١

إِن تَجْتَنِبُوا۟ كَبَآئِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ٣١

Na hili ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu na hisani yake juu ya waja wake Waumini. Aliwaahidi kwamba wakiepuka makubwa ya yale wanayokatazwa, atawafutia makosa yao madogo yote, na kuwaingiza pahali pa kuingia patukufu, penye heri nyingi. Nayo ni Pepo ambayo ndani yake kuna yale ambayo macho hayajawahi kuona, wala sikio halijawahi kusikia, wala hayajawahi kupita katika fikira za moyo wa mwanadamu yeyote. Na inaingia katika kuepuka madhambi makubwa kufanya mambo ya faradhi ambayo mwenye kuyaacha anakuwa amefanya dhambi kubwa, kama vile Swala tano, na Ijumaa, na Ramadhani. Kama alivyosema Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - “Swala tano, na Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani vinafuta yale yaliyo kati yake ikiwa makosa makubwa yataepukwa. Na bora zaidi katika maana za dhambi kubwa ni kwamba, dhambi kubwa ni ile ambayo ina adhabu maalum katika dunia au tishio la adhabu katika akhera; au kupinga kuwepo imani au kuiwekea laana au ghadhabu juu yake.