انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٨

يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ ٱلْإِنسَـٰنُ ضَعِيفًا ٢٨

{28} “Na Mwenyezi Mungu anataka kwamba awahafifishie.” Yani, kuwepesisha yale aliyowaamrisha na yale aliyowakataza. Kisha kutokea kwa ugumu katika baadhi ya sheria, aliwaruhusu kwa kiwango ambacho kinatakiwa na mahitaji yenu, kama vile mzoga, na damu, na mfano wa hayo kwa mwenye kulazimishwa. Na kama vile kumuoa mjakazi huru kwa masharti yale yaliyotangulia. Na hayo ni kwa sababu ya rehema yake kamili na wema wake wenye kujumuisha, na elimu yake, na hekima yake juu ya udhaifu wa mwanadamu katika nyanja zote. Udhaifu wa muundo, na udhaifu wa nia, na udhaifu wa azimio, na udhaifu wa imani, na udhaifu wa subira. Kwa hivyo, hayo yakawa mwafaka kwamba Mwenyezi Mungu amhafifishie kile anachodhoofika juu yake. Na kile ambacho imani yake, na subira yake, na nguvu zake haviwezi kustahimili.