انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢١

وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُۥ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَـٰقًا غَلِيظًا ٢١

{21} Yeye Mtukufu alieleza hekima ya hilo kwa kauli yake, "Na vipi mnaichukua ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?" Na ubainisho wa hilo ni kwamba mke kabla ya kufunga mkataba wa ndoa ni haramu kwa mume wake, naye hakuridhia kuwa halali kwake isipokuwa kwa mahari hiyo ambayo anampa. Kwa hivyo, akimjamii, na akawingilia, akampapasa kupapasa ambako kulikuwa haramu kabla ya hayo. Na ambako hakuridhia kumpa isipokuwa kwa badala hiyo, basi yeye pia ameshatimiza alichobadilisha kwa ajili yake, hivyo basi ikathibiti juu yake badala yake. Kwa hivyo, anawezaje kuchukua kwa badala kwa ukamilifu, kisha baada ya hilo anakirudia alichotoa kwa ajili ya badala hiyo? Hili ni katika dhuluma kubwa na ukandamizaji. Na vile vile kwa mkataba wa ndoa, Mwenyezi Mungu alichukua ahadi nzito kutoka kwa waume kwamba watatimiza haki za wake zao.