انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٦٧

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ قَدْ ضَلُّوا۟ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًا ١٦٧

{167} Alipojulisha kuhusu kuwatuma Mitume, swala na salamu za Mwenyezi Mungu ziwashukie, na akajulisha kuhusu kumtuma wa mwisho wao, Muhammad, na akaushuhudia juu yake, na Malaika wake wakaushuhudia, basi ikalazimu kutokana na hilo kwamba jambo lililothibitika na kushuhudiwa lithibitishwe. Basi ikawajibika kuwasadiki na kuwaamini, na kuwafuata. Kisha akamuahidi adhabu mwenye kuwakufuru, akasema, "Hakika, wale waliokufuru na wakazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu." Yaani, walijumuisha kati ya kukufuru wao wenyewe, na kuwazuia watu njia ya Mwenyezi Mungu. Na hawa [ndio] maimamu wa ukafiri na walinganiaji katika upotovu. "Hakika wamekwisha potea kupotea kwa mbali," na ni upotovu gani mkubwa zaidi ya upotovu wa mwenye kujipotoa mwenyewe na akawapotoa wengine. Basi akarejea na dhambi mbili hizo, na akarudi na hasara mbili hizo, na akakosa uwongofu huo uwili?