النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَبِظُلْمٍ مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَـٰتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ كَثِيرًا ١٦٠ وَأَخْذِهِمُ ٱلرِّبَوٰا۟ وَقَدْ نُهُوا۟ عَنْهُ وَأَكْلِهِمْ أَمْوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلْبَـٰطِلِ ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ١٦١
{160 - 161} Kisha Yeye Mtukufu akajullisha kuwa aliwaharimishia Watu wa Kitabu mazuri mengi ambayo yalikuwa halali kwao, na katazo hili ni adhabu kwa sababu ya dhuluma yao na kupita kwao mipaka. Na kuwazuilia kwao watu njia ya Mwenyezi Mungu, na kuwazuia kwao uwongofu, na kwa kuchukua kwao riba ilhali walikatazwa hilo, kwa hivyo wakawanyima haki watu masikini ambao wanafanya biashara nao. Basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa adhabu sawa na waliyoyafanya na akawakataza kutumia vitu vingi vyema ambavyo vilikuwa halali kwao na vilivyokuwa vizuri. Ama mambo ambayo yameharamishwa kwa umma huu (umma wa Muhammad), yameharamishwa ili kuwatakasa kutokana na machafu ambayo yanaweza kuwadhuru katika dini yao na dunia yao.