النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَسْـَٔلُكَ أَهْلُ ٱلْكِتَـٰبِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَـٰبًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا۟ مُوسَىٰٓ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوٓا۟ أَرِنَا ٱللَّهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ ٱتَّخَذُوا۟ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَءَاتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَـٰنًا مُّبِينًا ١٥٣ وَرَفَعْنَا فَوْقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَـٰقِهِمْ وَقُلْنَا لَهُمُ ٱدْخُلُوا۟ ٱلْبَابَ سُجَّدًا وَقُلْنَا لَهُمْ لَا تَعْدُوا۟ فِى ٱلسَّبْتِ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَـٰقًا غَلِيظًا ١٥٤ فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَـٰقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَقَتْلِهِمُ ٱلْأَنۢبِيَآءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌۢ ۚ بَلْ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ١٥٥ وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَـٰنًا عَظِيمًا ١٥٦ وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا ٱلْمَسِيحَ عِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ ٱللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا ٱتِّبَاعَ ٱلظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًۢا ١٥٧ بَل رَّفَعَهُ ٱللَّهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ١٥٨
{153 - 158} Swali hili lilitoka kwa Watu wa Kitabu kwa Mtume Muhammad - rehema na Amani zimshukie- kwa njia ya ukaidi na pendekezo, na kufanya kwao swali hili kuwa ndilo la kutegemea juu yake kuamini kwao au kukadhibisha kwao. Na hilo ni kwamba walimuuliza awateremshie Qur-ani kwa jumla moja, kama ilivyoteremka Taurati na Injili. Na hii ndiyo dhuluma kubwa zaidi kutoka kwao [na ujinga]. Kwa maana, Mtume ni mwanaadamu, mja anayeendeshwa, hana kitu mkononi mwake katika jambo hili, bali jambo lote ni la Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye anayetuma na anateremsha Apendavyo kwa waja wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Mtume alipotaja Aya ambazo washirikina walipendekeza wakimwambia Muhammad, "Sema: Subhana Rabbi (Ametakasika Mola wangu Mlezi!) Kwani mimi sikuwa tu isipokuwa ni mwanaadamu na Mtume?" Na vile vile kufanya kwao cha kutofautisha baina ya haki na batili kuwa ni kuteremshwa Kitabu kwa ujumla au katika nyakati tofauti tofauti, ni madai matupu ambayo hayana ushahidi wowote juu yake, wala hayafai, wala hata hakuna fikira yoyote potovu. Ni wapi inapatikana katika bishara ya yeyote katika Manabii kwamba, Mtume atakayewajia na kitabu kilichoteremshwa nyakati tofauti tofauti, basi msimwamini wala msimsadiki? Bali kuteremshwa kwa Qur-ani hii sehemu sehemu kulikuwa kulingana na hali, kitu kunachoashiria utukufu wake na uangalizi wa Mwenyezi Mungu kwa wale ambao iliteremshwa kwao. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na wakasema waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'ani kwa jumla moja? Hayo ni hivyo ili tuuthibitishe moyo wako, na ndiyo tumeisoma kwa mafungu. Wala hawatakuletea mfano wowote, ila na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora." Alipotaja pingamizi lao batili, akajulisha kuwa hilo si jambo geni katika mambo yao. Bali ilikwisha tokea kwao utangulizi mbaya, ambao ni mkubwa zaidi kuliko hayo waliyomfanyia yule Mtume ambaye wanadai kuwa wanamwamini. Kama vile kumuuliza wamuone Mwenyezi Mungu kwa macho yao, na kumfanya kwao ndama kuwa ni mungu kumwabudu baada ya yale waliyoona kwa macho yao miongoni mwa Ishara ambazo hakuna mwingine aliwahi kuziona. Na kama vile kukataa kwao kukubali hukumu za Kitabu chao, ambacho ni Taurati mpaka mlima ulipoinuliwa kutokea juu ya vichwa vyao, na wakatishiwa kwamba ikiwa hawataamini, basi utaangushwa juu yao, kwa hivyo wakakubali hayo kwa kuyafungia macho tu. Na kwa imani ambayo inafanana na Imani ya kulazimishwa, na kama vile kukataa kwao kuingia kwenye milango ya kijiji walichoamrishwa kuingia hali ya kuwa wamesujudu, na kwa kuomba kufutiwa dhambi. Lakini walihalifu kauli na vitendo. Na kama vile kupita mipaka kwa wale waliopita mipaka kuhusiana na siku ya Sabato, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa adhabu hiyo mbaya. Na kama vile kuchukua agano nzito kutoka kwao, lakini wakalitupa nyuma ya migongo yao, na wakakufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawaua Mitume Wake bila ya haki. Na kama vile kusema kwao kuwa hakika walimuua Masihi Isa na wakamsulubisha, ilhali hawakumuua, wala hawakumuua. Bali walifananishiwa asiyekuwa yeye, kwa hivyo wakamuua asiyekuwa yeye na wakamsulubisha. Na kama vile kudai kwao kwamba nyoyo zao zimefungwa, hazielewi hayo unayowaambia, wala hawazifahamu. Na kama vile kuwazuilia watu njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wakawazuilia haki, na kuwalingania kwa yale wanayoyaamini wao ya upotovu. Na kama vile kuchukua haramu na riba pamoja na Mwenyezi Mungu kuwakataza hayo, na kuyatilia mkazo. Basi wale waliofanya vitendo hivi haishangazi wao kumwomba Mtume Muhammad awateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na njia hii ni katika njia bora zaidi za kujadiliana na mpinzani mwenye batili. Nayo ni kwamba, linapotokea pingamizi la batili kutoka kwa mpinzani, ambalo alilifanya kuwa ndilo jambo lenye shaka kwake na kwa mtu mwingine ili kuikataa haki, basi inapaswa kueleza katika hali yake ovu na matendo yake mabaya ambayo ni mabaya zaidi kuliko yale yaliyotoka kwake. Ili ajue kila mmoja kwamba, pingamizi hili linatoka kwenye bonde lile la kudharauliwa, na kwamba lina utangulizi ambao hili linawekwa pamoja nao. Kadhalika, kila upinzani wanaopinga kwa huo unabii wa Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake - unaweza kukabiliwa na mfano wake au kitu chenye nguvu zaidi kuliko hicho katika unabii wa wale wanaodai kumwamini. Ili uovu wao utoshelezwe kwa hilo, na batili yao iweze kuangamizwa. Na kila hoja waliyoitumia katika kukiri kwao unabii wa yule waliyemwamini, basi hoja hiyo na mfano wake, na chenye nguvu zaidi kuiliko vinaashiria na kuthibitisha unabii wa Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake. Na kwa kuwa makusudio ya kuhesabu yale ambayo Mungu ameyataja katika machukizo yao haya ni kuyakabili, hakuyapanua pahali hapa, bali aliyaashiria tu na akayaelekeza katika sehemu zake. Na aliyapanua katika isiyokuwa sehemu hii, katika sehemu ifaayo kwa ajili ya kuyapanua.