انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤٥

إِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ فِى ٱلدَّرْكِ ٱلْأَسْفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ١٤٥

{145} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu hatima ya wanafiki kwamba wao watakuwa katika matabaka ya chini zaidi ya mateso, na hali mbaya zaidi za adhabu. Basi hao wako chini ya makafiri wengine wote. Kwa sababu, waliwashiriki katika kumkufuru Mwenyezi Mungu na kufanyia uadui Mitume wake, na wakawazidi kwa vitimbi na hadaa zao, na kuweza kuwafanyia Waumini aina nyingi za uadui kwa namna isiyotambulika wala kuhisiwa. Na wakaweza kupata kwa sababu ya hayo kuhukumiwa kwa hukumu za Uislamu na kustahiki yale ambayo hawakustahiki. Kwa hivyo, kwa sababu ya hayo na mfano wake, ndiyo wakastahiki adhabu kali kabisa. Na wala hawana mwokozi yeyote kutokana na mateso yake, wala wa kuwanusuru mwenye kuwazuia baadhi ya adhabu yake.