النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَن يَعْصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُۥ يُدْخِلْهُ نَارًا خَـٰلِدًا فِيهَا وَلَهُۥ عَذَابٌ مُّهِينٌ ١٤
{14} "Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake" n.k. Na inaingia katika neno maasia ukafiri na kilicho chini yake miongoni mwa maasia. Basi hakuna fikira potofu ndani yake kwa Makhawariji wanaosema kuwa watu wa madhambi ni makafiri. Kwani, Mwenyezi Mungu Mtukufu amefungamanisha kuingia Peponi na kumtii Yeye na kumtii Mtume wake. Na akafungamanisha kuingia Motoni na kumuasi Yeye na kumuasi Mtume wake. Basi mwenye kumtii kumtii kamili, ataingia Peponi bila ya kuadhibiwa. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake maasia kamili kwenye kuingiza ndani yake ushirikina na yale yaliyo chini yake, ataingia Motoni na atadumishwa humo. Na yule ambaye vitakutana ndani yake uasi na utiifu, atakuwa ndani yake na chenye kumsababishia kupata thawabu na adhabu kulingana na yaliyomo ndani yake ya utiifu na uasi. Na maandiko yaliyosimuliwa na idadi kubwa ya wale ambao hawawezi kukubaliana kudanganya yaliashiria kuwa, wale wanaomuabudu Mwenyezi Mungu peke yake ambao wana utiifu wa Tauhid hawatadumishwa Motoni. Kwa sababu kile walicho nacho cha Tauhidi kinawazuia na kudumu ndani yake.