انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢٠

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ إِلَّا غُرُورًا ١٢٠

{120} Kisha akasema, "Anawaahidi, na anawatia matumaini ya uongo." Yaani, Shetani anamuaahidi wale ambao anawafanyia juhudi ya kuwapoteza. Na ahadi hujumuisha ahadi ya mazuri na hata mabaya. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Shetani anawaahidi ufakiri;" kwani yeye anawaahidi wanapotoa katika njia ya Mwenyezi Mungu; kuwa watakuwa mafakiri, na inawatia hofu kwamba wakipigana Jihadi kwamba watauawa au mengineyo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Hakika huyo ni Shetani anayewatia hofu marafiki zake..." hadi mwisho wa Aya. Na huwatia hofu wanapopendelea radhi za Mwenyezi Mungu kwa kila linalowezekana na lisilowezekana, katika yale yanayoyaingiza kwenye akili zao, mpaka wanakuwa wavivu katika kutenda heri. Na vile vile anawapa matumaini ya uongo ambayo wakati yanapogundulika, yanakuwa kama sarabi ambayo haina uhakika wowote. Ndiyo maana akasema, “Na Shetani hawaahidi isipokuwa udanganyifu."