انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠٨

يَسْتَخْفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ ٱلْقَوْلِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ١٠٨

{108} Kisha ikatajwa juu ya hao wahaini kwamba “Wanawaficha watu, wala hawamfichi Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapopanga njama usiku kwa maneno asiyoyapenda.” Na hili ni katika udhaifu wa imani na upungufu wa yakini, kwamba iwe hofu juu ya viumbe kwao ni kubwa zaidi kuliko hofu ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wanafanya uangalifu kwa njia zinazoruhusiwa na zilizokatazwa ili wasifedheheke mbele ya watu. Nao pamoja na hilo wamemdhihirishia Mwenyezi Mungu mambo makubwa, na hawakujali kuwaangalia kwake na kujua kwake juu yake, naye yuko pamoja nao kwa elimu katika hali zao zote. Hasa katika hali ya kupanga njama usiku yale ambayo hayampendezi katika miongoni mwa kauli kama ile ya kumwachilia mwenye kosa, na kumtuhumu asiyekuwa na kosa, na kumfanyia juhudi Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ili afanye yale waliyopangia njama usiku. Basi hakika, walikusanya kati ya makosa kadhaa, na hawakumchunga Mola Mlezi wa ardhi na mbingu, anayeona siri zao na dhamiri zao. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu aliwaahidi adhabu kwa kauli yake, “Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka vyema wanayoyatenda,” yani alikwisha yazunguka hayo kwa elimu. Na pamoja na haya, hakuwaharakishia adhabu, bali aliwasubiria, na akawawekea toba, na akawaonya dhidi ya kuendelea juu ya dhambi zao zenye kusababisha adhabu kali.