انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠٤

وَلَا تَهِنُوا۟ فِى ٱبْتِغَآءِ ٱلْقَوْمِ ۖ إِن تَكُونُوا۟ تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ ۖ وَتَرْجُونَ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا يَرْجُونَ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ١٠٤

{104} Yani msidhoofike, wala msiwe wavivu katika kuwafukuzia maadui wenu miongoni mwa makafiri. Yani katika kupigana nao jihadi na kufanya ulinzi katika hayo. Kwa maana, udhaifu wa moyo husababisha udhaifu wa mwili, na hilo linafanya kuwa dhaifu katika kupambana na maadui. Lakini kuweni na nguvu na wakakamavu katika kuwapiga vita. Kisha akataja yale yanayotia nguvu nyoyo za waumini, na akataja mambo mawili: La kwanza ni kwamba yale yanayowapata miongoni mwa maumivu, na uchovu, na majeraha, na mfano wake, hayo pia yanawapata maadui zenu, kwa hivyo sio katika uungwana wa kibinadamu au uungwana wa Kiislamu kwamba muwe wadhaifu zaidi kuliko wao, na hali nyinyi na wao mko sawa katika yale yanayosababisha hayo. Kwa sababu, desturi iliyoenea ni kwamba hadhoofiki isipokuwa yule ambaye mateso yanampata kwa kufuatana, na maadui wake wakamshinda kwa daima, na siyo yule ambaye anashinda na anashindwa mara nyingine. Jambo la pili ni kwamba nyinyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu yale ambayo wao hawataraji. Mnataraji kufuzu kupata thawabu zake, na kuokoka kutokana na adhabu yake. Bali wale walio maalum miongoni mwa Waumini wana malengo ya juu zaidi, na matarajio makubwa zaidi kama vile kunusuriwa kwa Dini ya Mwenyezi Mungu, na kuisimamisha sheria yake, na kupanuka kwa duara ya Uislamu, na kuwaongoa waliopotea, na kuwazuia maadui wa Dini. Basi mambo haya yanamlazimu Muumini mkweli kuongeza nguvu, na kuongezeka ukakamavu wake, na ushujaa kamili. Kwa sababu, mwenye kupigana na akasubiri ili kupata utukufu wake wa duniani, akiupata, si kama mwenye kupigana kupata furaha ya kidunia na ya kiakhera na kufuzu kupata radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo yake. Basi, ametakasika Yule ambaye ametofautisha kati ya waja wake na akatengenisha kati yao kwa elimu yake na hekima yake, na ndio maana akasema. “Na hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.” Yani Mwenye elimu kamili, na hekima kamili.