انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَٰلَ ٱلْيَتَـٰمَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِى بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ١٠

{10} Na alipowaamrisha hayo, akawakemea dhidi ya kula mali za mayatima, na akawatishia adhabu kali zaidi kwa hayo. Akasema, “Hakika, wale wanaokula mali za mayatima kwa dhuluma,” yani, bila ya haki. Na kizuizi hiki kinatoa yale yaliyotangulia kuhusu masikini kuruhusiwa kula kwa wema, na kuruhusika kuchanganya mali zao na mali za mayatima. Kwa hivyo, mwenye kuila kwa dhuluma, basi hakika, “wanakula matumboni mwao moto.” Yani, hakika walichokula ni moto unaowaka ndani mwao. Nao ndio walioungiza katika matumbo yao. “Na wataingia Moto wenye mwako mkali.” Yani, moto unaochoma, uliookwa. Na hili ndilo tishio kubwa zaidi lililokuja kuhusiana na madhambi, linaloashiria uovu wa kula mali za mayatima, na ubaya wake, na kwamba hilo linasababisha kuingia motoni. Kwa hivyo, hilo likaashiria kuwa hilo ni miongoni mwa madhambi makubwa zaidi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu usalama.