الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالُوا۟ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى صَدَقَنَا وَعْدَهُۥ وَأَوْرَثَنَا ٱلْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ ٱلْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَآءُ ۖ فَنِعْمَ أَجْرُ ٱلْعَـٰمِلِينَ ٧٤
{74} "Nao watasema" watakapoingia na kutulia humo, wakimhimidi Mola wao Mlezi kwa yale aliyowaneemesha na aliyo na kuwaongoa: "Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetutimizia ahadi yake" ambayo ni Pepo kupitia ndimi za Mitume wake. Basi tukaamini na tukatengenea, naye akatutimizia yale aliyotuahidi "na akaturithisha ardhi" ya Peponi "tunakaa katika Bustani popote tupendapo." Yaani, tunaweza kwenda humo popote tunapotaka, na tunaweza kufurahia humo neema yoyote tunayoitaka, na hakuna kinachoweza kutuzuia tunachokitaka. "Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!" Wale waliofanya bidii katika kumtii Mola wao Mlezi katika muda mfupi wenye mwisho, kwa hivyo wakapata kwa sababu ya hilo heri kubwa yenye kudumu na kuendelea. Haya ndiyo makazi yanayostahiki kusifiwa kwa uhakika, ambayo hapo Mwenyezi Mungu atawatukuza viumbe wake maalumu, naye ambaye ni Mwenye kutoa kwa wingi akaridhia kwamba yawe mashukio yao. Alijenga sehemu ya juu yake, akaifanya kuwa nzuri zaidi, akaipanda kwa mkono wake, na akaijaza kwa rehema yake utukufu wake, kiasi kwamba mtu mwenye huzuni anafurahia kwa baadhi yake tu, dhiki yake inamtoka na utulivu unakamilika.