الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَقَدْ أُوحِىَ إِلَيْكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٦٥
{65} Ndiyo maana akasema: "Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako" miongoni mwa Manabii wote: "Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu matendo yako yataharibika." Hivi ndivyo Manabii wote waliwaambia watu wao kwamba ushirikina unaharibu matendo yote, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema katika Surat Al-An’am alipowahesabu wengi katika Manabii na Mitume wake, akasema kuwahusu: "Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo humuongoa amtakaye katika waja wake. Na lau wangelimshirikisha, basi yangeliwaharibikia waliyokuwa wakiyatenda." Na hapa akasema: "Na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kuhasiri" dini yako na akhera yako. Kwa hivyo, kwa kufanya ushirikina, matendo yanabatilika na mtu huyo anastahiki adhabu na mateso.