الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّهُۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ ٦٣
{63} "Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi." Anazijua na anazisimamia. "Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayoizuia hapana wa kuipeleka isipokuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Alipobainisha ukuu wake unaolazimu mioyo imtukuze kwa wingi na kumheshimu, akataja hali ya mtu aliyegeuza suala hili na hakumthamini anavyostahiki. Akasema: "Na wale waliozikataa Ishara za Mwenyezi Mungu" zinazoashiria haki ya yakini na njia iliyonyooka, "hao ndio wenye kuhasiri." Walihasiri yale ambayo kwayo nyoyo zanatengenea, kama vile kumfanyia Mwenyezi Mungu uungu na kumkusudia Yeye peke yake, na yale ambayo kwayo ndimi zinatengenea kama vile kuzishughulisha na kumtaja Mwenyezi Mungu, na yale ambayo kwayo viungo vinatengenea kama vile kumtii Mwenyezi Mungu. Wao walibadilisha hayo na wakaweka mahali pake kila chenye kuharibu nyoyo na miili, kwa hivyo wakakosa mabustani ya mbinguni ya neema na badala yake wakapata adhabu iumizayo.