الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسْرَفُوا۟ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا۟ مِن رَّحْمَةِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغْفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ ٥٣
{53} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawafahamisha waja wake waliopindukia mipaka juu ya ukubwa wa ukarimu wake, na anawataka watubie kabla ya kufikia hali ambayo hawataweza tena kufanya hivyo. Akasema: "Sema" ewe Mtume, na atakayeshika nafasi yako miongoni mwa wale wanaolingania Dini ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwapa habari waja juu ya Mola wao Mlezi: "Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao" kwa kufuata madhambi ambayo nafsi zao zinawaitia na kuwania katika mambo yanayomghadhibisha Mjuzi wa ghaibu zote, "Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu" mkajitia kwa mikono yenu katika maangamizo, na mkasema: Dhambi zetu zimekuwa nyingi na kasoro zetu zimeongezeka. Hakuna njia ya kuziondoa na wala hakuna njia ya kujiweka mbali nazo, na kwa sababu hiyo mkaendelea kufanya uasi wenu na mambo ya kumfanya Mwingi wa rehema kuwakasirikia. Lakini mjueni Mola wenu Mlezi kwa majina yake yanayoashiria ukarimu wake na kupeana kwake kwa wingi, na jueni kwamba Yeye anasamehe dhambi zote kama vile ushirikina, kuua, uzinzi, riba, dhuluma na madhambi mengineyo makubwa na madogo. "Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Yaani, hizi ndizo sifa zake za milele na kamwe haziachani naye. Athari zake zinaendelea kupatikana, zikijaza vilivyopo kwa heri usiku na mchana, na Yeye hutoa neema na fadhila kwa waja kwa siri na hadharani. Anapenda kutoa zaidi ya kuliko kuzuilia, na rehema yake ilitangulia na kushinda hasira yake.