الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّوْ أَرَادَ ٱللَّهُ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا لَّٱصْطَفَىٰ مِمَّا يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ ۖ هُوَ ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ ٤
{4} Yaani, "Lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka kuwa na mwana" kama wanavyodai hivyo baadhi ya watu wapumbavu, "basi bila ya shaka angeliteua amtakaye katika aliowaumba" na wala hangehitaji kuwa na mke. "Subhanahu (ametakasika)" mbali na hayo ambayo makafiri wanamdhania, au yale ambayo wavukao mipaka walimnasibisha nayo. "Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mshindi." Yaani, ni Mmoja katika dhati yake, katika majina yake, katika sifa zake na katika vitendo vyake. Hakuna afananaye naye katika chochote miongoni mwa hayo. Ikiwa angekuwa na mwana, basi hilo lingehitajika kwamba mwana huyo anafanana naye katika umoja wake; kwa sababu yeye alitokana naye na ni sehemu yake. Aliyeshinda ulimwengu wote,wa juu na wa chini.Ikiwa angekuwa na mwana, basi hangekuwa miongoni mwa walioshindwa, na angefanyiwa upole na baba yake. Umoja wake na ushindi wake ni mambo yasiyoachana. Kwa maana aliye Mmoja, hawi isipokuwa Mshindi kwa vyote. Naye Mshindi kwa vyote hawi isipokuwa Mmoja tu. Hayo yanapinga uwezekano wa kuwepo mshirika yeyote naye kwa namna zote.