انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزمر
السورة ٣٩

الزمر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٤

أَفَمَن يَتَّقِى بِوَجْهِهِۦ سُوٓءَ ٱلْعَذَابِ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ وَقِيلَ لِلظَّـٰلِمِينَ ذُوقُوا۟ مَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ٢٤

{24} Yaani, je, mtu huyu ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa na kumwezesha kufuata njia ifikishayo kwenye makao ya utukufu wake anatoshana na mtu aliye katika upotofu, na akaendelea na ukaidi wake mpaka ikafika Siku ya Kiyama? Basi ikamjia adhabu kubwa, kwa hivyo akaanza kujikinga kwa uso wake, ambao ndio kiungo cha heshima zaidi, na ambao hata adhabu ndogo tu inauathiri vibaya. Siku hiyo akawa anajikinga kwa uso wake kutokana na adhabu; kwani mikono yake na miguu yake itakuwa imefungwa pingu? "Na wataambiwa wenye kudhulumu" nafsi zao kwa ukafiri na maasia kwa njia ya kuwakaripia na kuwakemea: "Onjeni hayo mliyokuwa mkiyachuma!"