الزمر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَـٰكِنِ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ رَبَّهُمْ لَهُمْ غُرَفٌ مِّن فَوْقِهَا غُرَفٌ مَّبْنِيَّةٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ ۖ لَا يُخْلِفُ ٱللَّهُ ٱلْمِيعَادَ ٢٠
{20} Lakini kushinda kukubwa zaidi na kufuzu kukubwa zaidi ni kwa watu wema, ambao Mwenyezi Mungu amewaandalia mambo makarimu na neema mbalimbali ambazo kiwango chake hakiwezi kupimwa. "Watapata ghorofa" za juu, zilizopambwa miongoni kwa uzuri mkubwa, za kifahari kiasi kwamba nje yake inaweza kuonekana kutokea ndani yake na ndani yake kutokea nje yake. Na kutoka kwa kuinuka kwake juu sana zinaonekana kama nyota iliyo mbali zaidi katika upeo wa mashariki au magharibi, na ndiyo maana akasema: "zilizojengwa juu ya ghorofa" kwa dhahabu na fedha, na zimepakwa miski yenye harufu nzuri zaidi. "Chini yake hupita mito" inayotiririka, inayomwagilia bustani zenye maua na miti safi, inayotoa kila aina ya matunda matamu yaliyoiva. "Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake" aliyowaahidi wachamungu, kwa hivyo hakuna budi ataitimiza. Basi nawatimize sifa za uchamungu ili awalipe ujira wao.