ص
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ ٨٧
{87} "Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote." Ambayo kwayo wanakumbuka kila yenye kuwanufaisha miongoni mwa masilahi ya dini yao na dunia yao. Kwa hivyo ni utukufu na kunyanyuliwa kwa walimwengu, na pia ni hoja dhidi ya wakaidi. Sura hii kubwa inajumuisha ukumbusho wenye hekima, habari kuu, kusimamisha hoja na ushahidi juu ya wale wanaoikadhibisha Qur-ani, wanaoipinga na kumkadhibisha yule aliyekuja nayo. Na inapeana habari juu ya waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa, na malipo ambayo Mwenyezi Mungu atawalipa wacha Mungu na madhalimu. Ndiyo maana aliapa mwanzoni mwake kwamba Qur-ani hii ni yenye ukumbusho. Kama alivyosema: "Na umkumbuke mja wetu," na kauli yake: "Na wakumbuke waja wetu," na kauli yake: "kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho," na kauli yake: "Huu ni ukumbusho." Ewe Mwenyezi Mungu tufundishe katika Qur-ani hii yale ambayo hatuyajui, na utukumbushe yale tuliyoyasahau kwa njia ya kughafilika na kuwa katika njia ya kuyaacha.