ص
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ٨٢ إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ ٱلْمُخْلَصِينَ ٨٣
{82 - 83} Alipojua kwamba amepewa muhula, akamuonyesha Mola wake Mlezi ukubwa wa uadui wake kwake na kwa Adam na kizazi chake.Akasema: "Ninaapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote." Inawezekana kwamba “ba” iliyotumika hapa ni ile ya kuapia. Na kwamba aliapa kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu kwamba atawapoteza wote; "Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliosafishwa." Hao alijua kwamba Mwenyezi Mungu atawalinda kutokana na vitimbi vyake. Na inawezekana kwamba "ba" hii ni ile inayotumiwa katika kutafuta msaada wa kitu fulani. Na kwamba alipojua kuwa hana uwezo kwa namna zote, na kwamba hataweza kumpoteza yeyote isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, akatafuta msaada kutoka kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu ili kukipoteza kizazi cha Adam. Huyu kwa hakika ndiye adui wa Mwenyezi Mungu. Nasi, ewe Mola wetu Mlezi, ni wanyonge na wasioweza kutekeleza mambo vilivyo, ambao tunakiri kila neema yako; kizazi cha yule uliyemtukuza na kumkirimu. Basi tunaomba msaada kutoka kwa utukufu wako mkubwa, uwezo wako na rehema yako iliyoenea kila kiumbe. Rehema ambayo kwayo umetufikishia neema mbalimbali za kidini na za kidunia, na ambayo kwayo ulituepusha adhabu mbalimbali kwamba utusaidie kupigana naye na utusaidie dhidi ya uadui wake. Na utuweke salama kutokana na uovu wake na shirki yake. Na tuna imani na Wewe kwamba utatuitikia dua zetu na tunaamini ahadi yako uliyotuambia: "Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni." Basi, tumeshakuomba kama ulivyotuamrisha, kwa hivyo tuitikie kama ulivyotuahidi. "Hakika Wewe huvunji miadi yako."